Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MFUKO WA MISITU TANZANIA(TaFF)

MAFUNZO KWA WANUFAIKA WAPYA WA RUZUKU

Imewekwa: 10 April, 2025
MAFUNZO KWA WANUFAIKA WAPYA WA RUZUKU

Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) umefanya mafunzo kwa wanufaika wapya wa ruzuku kwa lengo la kujengea uelewa wa utekelezaji wa mradi wa ruzuku. Katika mafunzo hayo wanufaika wamefundishwa juu ya:

  • Maelezo kwa ufupi kuhusu Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF)
  • Kupitia vifungu vya mkataba wa utoaji ruzuku
  • Namna ya kutaarisha/ kuandaa muktasari wa mradi
  • Namna ya kutayarisha / kuandaa taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi
  • Namna ya kutayarishwa / kuanza taarifa ya matumizi ya fedha za ruzuku
  • Aina ya stakabadhi / risiti zinazohitajika kufanyia marejesho ya matumizi ya fedha za ruzuku
  • Kupitia rasimu za mikataba