Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MFUKO WA MISITU TANZANIA(TaFF)

Kutoa Ruzuku

Mfuko wa Misitu Tanzania unatoa uwezeshaji kupitia utoaji ruzuku kwa mujibu wa Kanuni za misitu za utoaji ruzuku zinazojulikana kwa lugha ya kiingereza kama “The Forest (Manner and Criteria for Awarding Grants) Regulations, 2021”. Kwa mujibu wa Kanuni hizo,ruzuku hutolewa baada ya kuwasilishwa kwamaombi kwakuzingatiavipaumbele vyamwaka husika, na maombi yawe yamekidhi vigezo na masharti ya kupatiwa ruzuku. Kupitia tangazo hili, wadau wenye sifa wanaalikwa kuwasilisha maandiko kwa ajili ya kuomba ruzuku.Aidha, kwa waombaji wa ruzuku ndogo, ruzuku ya kati na ruzuku kubwa kuna dirisha moja tu la kupokea maandiko ya kuomba ruzuku ambapo mwisho wa kupokea maombi ya ruzuku ndogo, ruzuku ya kati na ruzuku kubwa ni tarehe 31 Machi, 2025. Maandiko yatakayowasilishwa baada ya tarehe hiyo hayatashughulikiwa. Jedwali Na. 1 linaonesha hatua na mtiririko wa kuwasilisha na kushughulikia maombi ya ruzuku.

JedwaliNa.1: Hatua na mtiririko wa kuwasilisha maombi hadi utoaji wa ruzuku

Muda

Shughuli

Mhusika

Desemba

Kutolewa kwa tangazo la kuitisha maandiko ya kuomba ruzuku

Sekretarieti ya Mfuko wa Misitu Tanzania

Januari hadi Machi

Kuandaa na kuwasilisha maandiko ya kuomba ruzuku

Waombaji wa ruzuku

Mwisho wa mwezi Machi

Mwisho wa kuwasilisha maandiko ya kuomba ruzuku

Waombaji wa ruzuku

Aprili hadi Juni

Uchambuzi wa awali wa maandiko ya kuomba ruzuku

Sekretarieti ya Mfuko

Uchambuzi wa kina wa maandiko ya kuomba ruzuku

Kamati ya Uchambuzi

Julai hadi Agosti

Uwasilishaji wa taarifa ya uchambuzi wa maandiko ya kuomba ruzuku

Kamati ya Uchambuzi

Uhakiki wa miradi iliyopendekezwa kupatiwa ruzuku

Sekretarieti ya Mfuko

 

Septemba

Uamuzi wa utoaji wa ruzuku

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko

Kuwajulisha waombaji kuhusu uamuzi kuhusu maombi yao ya ruzuku

Sekretarieti ya Mfuko

 

Oktoba

Mafunzo kwa wanufaika wapya wa ruzuku

Sekretarieti ya Mfuko na      Wanufaika wa ruzuku

Kuandaa na kusaini mikataba ya utoaji ruzuku

Novemba

Kutoa malipo ya awamu ya kwanza

Sekretarieti ya Mfuko

Kuanza kwa utekelezaji wa miradi iliyopatiwa ruzuku

Wanufaika wa zuzuku