Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MFUKO WA MISITU TANZANIA(TaFF)

DKT. MSUYA AIPONGEZA FITI KWA USIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI WA HOSTEL

Imewekwa: 01 October, 2026
DKT. MSUYA AIPONGEZA FITI KWA USIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI WA HOSTEL

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), Dkt. Tuli Salum Msuya, amekipongeza Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) kwa usimamizi wa mradi wa ujenzi wa jengo la hostel unaofadhiliwa na Mfuko huo, akieleza kuwa usimamizi wa mradi ni sehemu muhimu katika kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Dkt. Msuya ametoa pongezi hizo leo, Septemba 30, 2026, alipotembelea eneo la mradi chuoni hapo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi na kujionea utekelezaji wa mradi huo.

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia mradi kwa kuzingatia ubora wa ujenzi, matumizi sahihi ya fedha na muda uliopangwa ili kuhakikisha jengo hilo linakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wanafunzi.

Mradi huo wa ujenzi wa hostel ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu ya Chuo cha Viwanda vya Misitu na kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

slot gacor