Ruzuku Maalum
Kiasi cha fedha zaidi ya Shilingi Milioni 50 na walengwa wake ni Taasisi za Serikali tu ambazo zitatekeleza miradi ya kimkakati yenye mchangomkubwa katika uhifadhi,usimamizi nauendelezaji warasilimalimisitu.Miradiinayoweza kupatiwa ruzuku maalum ni miradi ya uanzishwaji na uendelezaji wa mashamba ya miti ya kupanda; kuboresha ufugaji nyuki na kujenga uwezo wa Taasisi za Serikali za Mafunzo na Utafiti za sekta ya misitu na nyuki zilizo chini ya Wizara ya Maliasili naUtalii. Maandiko ya kuomba ruzuku yanaweza kuwasilishwa wakati wowote lakini uchambuzi wa maombi ya ruzuku utafanyika kila baada ya miezi mitatu. Aidha, ruzuku maalum ni kwa ajili ya miradi ambayo utekelezaji wake unaweza kuchukua hadi miaka mitatu (miezi 36).