Ruzuku ndogo ambayo imegawanyika katika makundi mawili:
Kiasi cha fedha kisichozidi Shilingi Milioni Tano (TZS 5,000,000). Walengwa katika kundi hili ni watu binafsi ambao wana maeneo yasiyopungua ekari 10 na wameanza shughuli za upandaji miti. Aidha, Wanachuo wanaosoma Shahada ya Uzamili (Masters Degree) na Shahada ya Uzamivu (PhD Degree) wanaweza kuomba ruzuku ndogo ya kundi hili kwa ajili ya kutekeleza miradi ya utafiti inayohusiana na misitu au ufugaji nyuki ambayo inatokana na maandiko ya utafiti wa masomo yao.Vilevile, shule za msingina sekondari ni walengwa wa kundi hili la ruzuku kwa ajili ya kutekeleza miradi ya uanzishwaji wa vitalu vya miti shuleni na upandaji miti katika maeneo ya shule na maeneo ya jirani.
Kiasi cha fedha zaidi ya Shilingi Milioni Tano (TZS 5,000,000) lakini hakizidi Shilingi Milioni 10 (TZS 10,000,000). Walengwa katika kundi hili ni vikundi vya kijamii na ruzuku hii ni kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya upandaji miti au ufugaji nyuki. Kundi hili la ruzuku ni mahususi kwa CBOs, hivyo watu binafsi na makundi mengine sio walengwa wa ruzuku hii.
Ruzuku ndogo ni kwa ajili ya miradi ambayo utekelezaji wake unaweza kuchukua hadi miezi 12.