Top
  • The United Republic of Tanzania

    Ministry of Natural Resources and Tourism

    Tanzania Forest Fund-TaFF

DED MBOZI AISHUKURU TaFF KWA KUTOA RUZUKU YA VIFAA KWA VIKUNDI 10

Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde ameushukuru Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) kwa kuwapatia ruzuku ya vifaa vikundi 10 katika Halmashauri hiyo.

Nandonde alitoa shukrani hizo  Jumanne Junuari 2, 2024, wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa kwaajili ya kuwezesha vikundi vya ufugaji nyuki kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa lengo la kuboresha Maisha ya jamii hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Nandonde amesema kuwa kuna kasumba ya Watanzania wengi wakipewa vitu vya ruzuku hawafanyi vizuri na kufanya lengo la Serikali lililokusudiwa kutofikiwa.

‘’Leo tumepewa vifaa hivi nendeni mkafanyie kazi iliyokusudiwa kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kujiingizia kipato, vifaa hivi msiviuze na mkitumia vizuri vitaleta tija kwasababu masoko ya asali yapo" amesema

Kwa upande wake Katibu Tawala Mfuko wa Misitu Tanzania Dkt.Tuli Msuya amesema kuwa kutokana na kuwakabidhi vifaa hivyo ni matarajio ya Serikali kuona wanakikundi hao kuanza kuzalisha asali kwa wingi na bahati nzuri soko la asali lipo jirani katika mji wa Tunduma

‘’Serikali inaingia gharama kubwa kwaajili ya ununuzi wa vifaa hivyo, naomba msiende kubadilisha matumizi ya vifaa hivyo’’ alisisitiza

Dkt. Msuya alisema mradi ulikuwa unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza wanakikundi walipewa mizinga 400, na kwa awamu ya pili wamekabidhiwa mavazi na vifaa vingine vya ufugaji nyuki ikiwemo bomba la kufukiza moshi, Mabuti, glovu, tochi na mashine mbili kwaajili ya kuchujia asali.

Kwa upande wake mmoja wa wanakikundi hao Absolom amesema kuwa kutokana na kupewa vifaa hivyo wataweza kuongeza mizinga mingine na kuzalisha kwa wingi asali na pia watahamasika kupanda miti mingine kwa wingi ili kuhifadhi misitu.