Top
  • The United Republic of Tanzania

    Ministry of Natural Resources and Tourism

    Tanzania Forest Fund-TaFF

Dhamira ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) ni kuhakikisha upatikanaji wa fedha na kuwezesha na kugharamia ulinzi, uhifadhi, usimamizi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali misitu hapa nchin

Dhamira ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) ni kuhakikisha upatikanaji wa fedha na kuwezesha  na kugharamia ulinzi, uhifadhi, usimamizi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali misitu hapa nchini. Pichani ni wanavikundi kutoka vijiji  vya Mazingara na Suwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakiandaa mizinga ya nyuki (wakifanya uambikaji) kwa ajili ya kutundikwa. Mzinga hiyo ya nyuki wamepatiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Handeni kupitia mradi wa kuwezesha ufugaji nyuki uliopatiwa ruzuku na Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF). Ufugaji nyuki unachangia uboreshaji wa uhifadhi wa rasilimali misitu kwa kuwa jamii inapata chanzo mbadala cha mapato na hivyo kupunguza utegemezi wa misitu katika kujipatia kipato.