Top
  • The United Republic of Tanzania

    Ministry of Natural Resources and Tourism

    Tanzania Forest Fund-TaFF

ZIARA YA BODI YA WADHAMINI WA MFUKO WA MISITU TANZANIA TaFF KWENYE UJENZI WA KIWANDA CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOMBE JUNI, 2023

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti Bodi hiyo Prof. Shabani A. Chamsama wametembelea Kiwanda cha Kuchakata Mazao ya Nyuki Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Tarehe 08 Juni, 2023.  

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imepata ruzuku kutoka kwa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kiwanda na ununuzi wa mitambo ya kiwanda ya kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki. Bukombe ambayo inatekeleza mradi huo katika eneo la Ushirombo kata ya Katente ilipokea kiasi cha ruzuku ya dhamani ya Tsh 530,640,514/= kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania walitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kwa Lengo la Kukagua Utekelezaji wa Thamani ya Fedha za Ruzuku Zilizotolewa na Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF).

Kwa Picha zaidi Tembele: https://www.mfukowamisitu.go.tz/index.php/newsroom/gallery/ziara-ya-bodi-kiwanda-cha-kuchakata-mazao-ya-nyuki-halmashauri-ya-wilaya-ya-bukombe-juni-2023