Top
  • The United Republic of Tanzania

    Ministry of Natural Resources and Tourism

    Tanzania Forest Fund-TaFF

MFUKO WA MISITU TANZANIA WASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA JIJINI MBEYA

Bw Juma Ally, Afisa Miradi akieleza shughuli zinazofanywa na Mfuko wa Misitu Tanzania mbele ya Mdau katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea Jijini Mbeya.

Wadau wote mnakaribishwa kujua fursa za Mfuko wa Misitu Tanzania. Tupo ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) unaendelea kutoa elimu kuhusu fursa za uwezeshaji unaotolewa na Mfuko na utaratibu wa kuomba ruzuku katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea Jijini Mbeya. Picha inaonesha Afisa Miradi wa Mfuko wa Misitu Tanzania Bw. Juma Ally akitoa maelezo kwa wadau waliotembelea banda la Mfuko lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.

Afisa TEHAMA wa Mfuko wa Misitu Tanzania akitoa Elimu ya Mfumo wa Kuomba Ruzuku kwa Mdau katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea Jijini Mbeya. Wadau wote mnakaribishwa kupata elimu ya matumizi ya Mfumo wa Kuomba Ruzuku TaFF, Tupo ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.