Top
  • The United Republic of Tanzania

    Ministry of Natural Resources and Tourism

    Tanzania Forest Fund-TaFF

BODI YA WADHAMINI YAFANYA UKAGUZI WA MIRADI ILIYOPATIWA RUZUKU NA MFUKO WA MISITU TANZANIA

Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) umewezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali na kwa nyakati tofauti kikiwepo Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora (BTI). Chuo kiliomba fedha kwa lengo la 

  1. Mradi wa Ukarabati wa Jengo la Utawala

Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora (BTI) kiliomba Mfuko jumla ya TZS 150,000,000.00 kwa ajili ya mradi huu na kupatiwa fedha yote kiasi cha shilingi 150,000,000.00/= na Mfuko wa Msitu Tanzania kwa lengo la kutekeleza mradi huu. Chuo kimetumia TZS 85,579,101.26 hadi kukamilika kwa mradi. Aidha, kwa utaratibu huo jumla ya TZS 64,420,898.74 zilikuwa ni bakaa kutoka TZS 150,000,000.00 za ruzuku ya Mfuko na zilitumika kwenye jengo jipya la Utawala.

Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) wakiwa na Menejimenti ya Chuo cha Mfunzo ya Ufugaji Nyuki (BTI) mbele ya jengo la utawala baada ya ukaguzi wa ukarabati wa jengo hilo.


  1. Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Kuchakata Mazao ya Nyuki

Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora (BTI) kiliomba jumla ya TZS 199,996,879.00 kutoka kwa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) kwa ajili ya mradi huu, na kupokea fedha asilimia mia moja kwa awamu husika kutoka Mfuko. Aidha, mradi huu umekamilika kwa asilimia 100% ikiwa ni pamoja na kufunga mitambo ya kuchakatia mazao ya nyuki ambayo ilifadhiliwa na TaFF.

Bodi ya Wadhamini wakipata elimu ya namna mitambo ya kuchakata asali inavyofanya kazi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki (BTI) Mkoani Tabora.

Katibu Tawala wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) akishikilia moja ya bidhaa iliyozalishwa na mitambo ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki (BTI) iliyofadhiliwa na Mfuko.

 

Kwa Picha Zaidi Tembelea: https://www.mfukowamisitu.go.tz/index.php/newsroom/gallery/ziara-chuo-cha-mafunzo-ya-ufugaji-nyuki-tabora-bti